KOZI YA SHAHADA KWA MWAKA WA MASOMO 2017/2018

 

Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika kilichopo Changanyikeni Dar es Salaam anapenda kuwatangazia wazazi na wanafunzi wote nafasi za masomo ya Shahada (Bachelor Degree) ya Takwimu Rasmi kwa mwaka 2017/2018.

 

Chuo kimeaanza kupokea maombi ya udahili wa wanafunzi kuanzia tarehe 22 Julai, 2017 hadi tarehe 30 Agosti, 2017. Masomo kwa mwaka 2017/2018 yanatarajiwa kuanza rasmi tarehe 30 Octoba, 2017.

 

SIFA ZA KUJIUNGA

 

• Mwombaji awe mhitimu wa Kidato cha SITA ( katika masomo ya Sayansi au Biashara; ikiwa ni pamoja na Subsidiary katika somo la BAM) mwenye ufaulu wa angalau    point 4 pamoja na ufaulu wa angalau kuanzia D nne katika kidato cha Nne yakiwemo masomo ya Hesabu na Kiingereza kwa mchanganuo ufuatao;

      i. DD au zaidi kwa wale walio maliza kabla ya mwaka 2014

     ii. CC au zaidi kwa walio maliza kati ya mwaka 2014 – 2015.

    iii. DD au zaidi kwa wale walio maliza kuanzia mwaka 2016

 

• Mwombaji awe na Diploma katika masomo ya Sayansi, Biashara, Uhasibu (GPA 3 au zaidi) akiwa na D nne kidato cha Nne ikiwemo ya kiingereza na Hesabu au NVA level 3.

 

Chuo cha Takwimu Mashariki Mashariki mwa Afrika, Ni chuo cha Serikali na kimeanza kutoa mafunzo ya takwimu rasmi kuanzia mwaka 1965, kina ithibati ya NACTE na TCU na ni chuo pekee kinachotoa mafunzo ya Takwimu Rasmi katika ngazi za,Astashahada (Certificate), Stashahada (Diploma),Shahada (Bachelor Degree), na Shahada ya Uzamili (Masters Degree) ya Takwimu Rasmi Afrika.

 

Maombi yote yafanywe kupitia Online Application System (OLAP) katika website ya chuo ambayo ni www.eastc.ac.tz. au fika chuoni kwa msaada zaidi . Ada ya maombi ni Tsh. 10,000/= na ada kwa mwaka ni Tsh. 1,125,000/= .

 

Unaweza kupata maelezo zaidi kupitia info@eastc.ac.tz au kwa kupiga simu 0784 784 106

 

Jina la Account: EASTC

Jina la Bank: CRDB

Namba ya Account: 0150396002400

 

 

image: