KOZI ZA ASTASHAHADA NA STASHAHADA KWA MWAKA WA MASOMO 2017/2018.

 

Mkuu wa Chuo cha Takwimu cha Mashariki mwa Afrika kilichopo Changanyikeni Dar es Salaam anapenda kuwatangazia wazazi na wanafunzi wote nafasi za masomo ya Astashada (Certificate) na Stashahada (Diploma) ya Takwimu kwa mwaka 2017/2018.

 

Chuo kimeaanza kupokea maombi ya udahili wa wanafunzi kuanzia tarehe 15 Mei, 2017 hadi tarehe 20 Agosti, 2017. Masomo kwa mwaka 2017/2018 yanatarajiwa kuanza rasmi tarehe 25 Septemba, 2017.

 

SIFA ZA KUJIUNGA

Mafunzo ya Astashahada (Certificate) ya Takwimu (mwaka mmoja):

  • Mwombaji awe amehitimu Kidato cha Nne akiwa na ufaulu wa ‘D’ nne ikiwemo ya Hisabati na Kiingereza.

 

 

Mafunzo ya Stashahada (Diploma) ya Takwimu (miaka miwili)

  • Mwombaji awe mhitimu wa Kidato cha Sita:akiwa na ufaulu wa ‘E’ somo la Hisabati au ‘S’ katika somo la BAM (Basic Applied Mathematics) AU
  • Mwombaji awe mhitimu wa Kidato cha nne chenyeufaulu wa D nne na Cheti cha Astashahada kutoka Chuo kinachotambulika na NACTE.

 

 

Chuo kina ithibati ya NACTE, na ni chuo pekee kinachotoa mafunzo ya Takwimu Rasmi katika ngazi za Cheti Maalumu cha Ukusanyaji wa Takwimu (Certificate in Data Collection),Astashahada (Certificate), Stashahada (Diploma),Shahada (Bachelor Degree), na Shahada ya Uzamili(Masters Degree) ya Takwimu Rasmi.

 

Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti hii www.eastc.ac.tz aupiga simu 0784 784 106

 

Maombi yatumwe kupitia tovuti ya EASTC ambayo ni www.eastc.ac.tz

 

image: