MAFUNZO MAALUMU YA CHETI CHA UKUSANYAJI TAKWIMU ( BATCH 11)

Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) inapenda kuwajulisha wananchi wote kuwa mtu yeyote anayetaka kuwa Mdadisi au Mkusanyaji taarifa za kitakwimu rasmi katika tafiti mbalimbali zinazoratibiwa na ofisi hii, ni sharti awe amehitimu Mafunzo ya Ukusanyaji Takwimu Rasmi angalau kwa ngazi ya cheti.

 

Hii ni kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu Na. 9 ya mwaka 2015 inayoipa mamlaka Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya kuratibu na kusimamia ukusanyaji takwimu rasmi (official statistics) nchini. 

 

Hivyo, kuanzia sasa NBS itakuwa inawatumia wadadisi ambao wamehudhuria na kuhitimu angalau cheti cha Ukusanyaji Takwimu Rasmi katika miradi mbalimbali ili kuboresha zaidi upatikanaji wa takwimu bora rasmi nchini.

 

Mafunzo ya Ukusanyaji Takwimu Rasmi yanatolewa na Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika “Eastern Africa Statistical Training Centre” (EASTC) kilichopo Changanyikeni jijini Dar es Salaam.

Kwa mawasiliano zaidi na kujisajili wasiliana na:

Ofisi ya Msajili wa Chuo,

Chuo cha Takwimu Mashariki mwa AfrikaEastern Africa Statistical Training Centre,

S.L.P 35103,

DAR ES SALAAM.

Barua pepe: info@eastc.ac.tz;

Tovuti: www.eastc.ac.tz  

Simu namba: 022-2925000 au 0784784106.

Tangazo hili limetolewa na:      

Mkurugenzi Mkuu,

Ofisi ya Taifa ya Takwimu,

DAR ES SALAAM.

05 Oktoba, 2016.

 

------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

 

Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika “Eastern Africa Statistical Training Centre” kilichopo Changanyikeni Dar es Salaam, anatangaza mafunzo maalumu ya Ukusanyaji Takwimu Rasmi kwa ngazi ya cheti kwa mtu yeyote anayetaka kuwa Mdadisi au Mkusanyaji taarifa za kitakwimu katika tafiti mbalimbali ili kuboresha zaidi Taaluma ya ukusanyaji Takwimu Rasmi.

 

Sifa za muombaji:
  • Awe amemaliza kidato cha nne; au
  • Awe alishawahi kufanya angalau tafiti moja inayosimamiwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu.
Muda wa Mafunzo:
  • Mafunzo haya ni ya muda wa miezi miwili tu,
  • Mafunzo haya yataanza rasmi tarehe 19th February 2018, Chuoni EASTC.
  • Kwa waliohitimu kidato cha nne mwaka 2017 tunawapokea.
Mwisho wa Maombi:
  • Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 17th February 2018
  • Maombi yatumwe kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya chuo ambayo ni: www.eastc.ac.tz/
Jinsi ya kuomba:
  • Maombi yatumwe kwa njia ya mtandao kupitia Tovuti ya chuo ambayo ni: www.eastc.ac.tz/cut au fika chuoni kwa msaada zaidi.

 

Kwa Mawasiliano zaidi na Kujisajili Wasiliana na:

  • Ofisi ya Msajili wa Chuo,

         Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika   

         (EASTC),

         S.L.P 35103,

         DAR ES SALAAM.

         Barua pepe: info@eastc.ac.tz  

         Tovuti: www.eastc.ac.tz

         Simu nambari: 022-2925000 au 0784784106.

 Ada na Malipo Mengine  >> Bonyeza Hapa <<

 

Note

Malipo yote yafanyike kupitia akaunti ya chuo ( EASTC ) iliyoko benki ya CRDB kwa kuandika yafuatayo;

JINA : EASTERN AFRICA STATISTICAL TRAINING CENTRE

JINA LA BENKI : CRDB BANK, UDSM BRANCH

NAMBA YA AKAUNTI : 0150396002400

FEDHA : TZS

SWIFTCODE : CORUTZTZ

 

 

Tangazo hili limetolewa na: 

Mkuu wa Chuo,

Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika,

DAR ES SALAAM.

 

Jinsi ya kufika Chuoni: BONYEZA HAPA