TANGAZO LA KAZI ZA WADADISI (NAFASI 450)

Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) inawatangazia watanzania wenye sifa kuomba kazi ya muda ya udadisi au ukusanyaji wa takwimu nafasi 450 kwa ajili ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi wa mwaka 2017/18  (Household Budget Survey) utakaofanyika katika mikoa yote ya Tanzania Bara. Utafiti huu unahitaji mwombaji atoke kwenye eneo ambalo utafiti unafanyika na awe tayari kufanya kazi kwa kipindi chote cha miezi 12. Sifa za mwombaji  zinazohitajika pamoja na maeneo yaliyochaguliwa  kwa ajili ya utafiti huu yameanishwa kwenye tangazo la kazi ambalo linapatikana kwenye kila Ofisi ya Mkoa ya Ofisi Taifa ya Takwimu.

 

Barua ya maombi ya kazi itumwe kwenye Ofisi ya NBS ya Mkoa ambako unaishi. Maombi yanatakiwa yatumwe kabla ya  tarehe 12 Agosti, 2017

                                                                       

      NB:  i. Tangazo hili linapatikana kupitia www.nbs.go.tz pamoja na www.eastc.ac.tz

               ii. Wale watakaochaguliwa kwa ajili ya usaili ndio watakaoitwa. NBS haitahusika na   gharama za kuja kwenye usaili huu.

 

IMETOLEWA NA

MKURUGENZI MKUU

OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU

27 Julai, 2017

image: