TANGAZO LA NAFASI ZA MASOMO KWA AWAMU YA PILI KWA MWAKA 2017/2018 CHUO CHA TAKWIMU MASHARIKI MWA AFRIKA

Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika kilichopo Changanyikeni Dar es salaam anapenda kuwatangazia wazazi na wanafunzi wote nafasi za masomo ya Astashada (Certificate) na Stashahada (Diploma) ya Takwimu kwa  mwaka 2017/2018 awamu ya pili.

 

Chuo  kimeaanza kupokea maombi ya udahili wa wanafunzi kuanzia tarehe 18 September, 2017 hadi tarehe 29  September, 2017 .

 

SIFA ZA KUJIUNGA

 

A: CERTIFICATE

Kwa wahitimu wa kidato cha nne wanatakiwa awe na ufaulu angalau ‘D’ nne ikiwemo ya hesabu na kiingereza.

 

B:  DIPLOMA

Kwa wahitimu wa kidato cha sita wanatakiwa wawe na ufaulu angalau  ‘E’ katika somo la hisabati au ‘S’ katika somo la BAM (Basic Applied Mathematics) au ufaulu wa Cheti kutoka Vyuo vinavyotambulika na NACTE.

 

Chuo kina ithibati ya NACTE, na ni  Chuo pekee kinachotoa mafunzo ya Takwimu Rasmi katika ngazi za Astashahada (certificate), Stashahada (Diploma), Shahada (Degree), na  Shahada ya uzamili(Masters)

 

Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti hii  www.eastc.ac.tz au piga simu 0784 784 106 

Maombi yatumwe kupitia tovuti ya EASTC ambayo ni www.eastc.ac.tz/apply

 Ada ya maombi ni tsh.10,000/=

Malipo yote yafanyike kupitia :

Jina la Akaunti:                     EASTC

Namba ya Akaunti:               0150396002400

Jina la Benki:                        CRDB

image: