TANZANIA UNION OF GOVERNMENT AND HEALTH EMPLOYEES (TUGHE)
UTANGULIZI
Chama cha wafanyakazi wa serikali kuu na Afya Tanzania (TUGHE) kina kauli mbiu isemayo "Huduma Bora na Maslahi zaidi".
HAKI ZA MWANACHAMA
Mwanachama yeyote, mbali na wanachama wa heshima, atakuwa na haki zifuatazo:-
- Kuwakilishwa na Chama dhidi ya mwajiri wake pamoja na haki ya yeye mwenyewe kujitetea dhidi ya mwajiri huyo kwa mashtaka yoyote dhidi yake.
- Kujitetea mbele ya vyombo mbali mbali vya chama na haki ya kuomba rufaa katika vyombo vya juu vya chama pale ambapo itabidi kama hataridhika na uamuzi uliotolewa.
- Kuwa na haki ya kushiriki katika uchaguzi wa viongozi wa chama kwa mujibu wa katiba zilizopo.
IMANI YA TUGHE
Chama kinaamini kuwa:-
- Wafanyakazi wote duniani ni sawa.
- Kila mfanyakazi anastahili malipo ya haki kufuatana na jasho lake na kuheshimiwa kama binaadamu.
- Ushikamano wa wafanyakazi wote duniani ndio njia pekee itakayo kuza ushirikiano wa karibu kati ya wafanya kazi na vyama vyao katika nchi zote.
- Kila mfanyakazi atakua huru kujiunga na chama chochote cha siasa atakachopendelea.
UONGOZI WA TUGHE-EASTC
TUGHE-EASTC ni Tawi la TUGHE ambalo lina uongozi kamili wa kiutawala kwa ngazi ya Tawi.
VIONGOZI WAKUU WA TUGHE-EASTC.
- Hassan Ramadhan Joho (Mwenyekiti).
- Ali Swalehe Mapui (Katibu).
WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU.
- Nelson J. Ndifwa (Mjumbe).
- Shaweji Twaibu (Mjumbe).
- Rita Maro (Mjumbe).
REJEA:
- Kadi ya Mwanachama TUGHE.
- Office ya TUGHE-EASTC.
ANUANI:
Katibu: Ali Swalehe Mapui.
Email:mapui@live.com
Tel: +255-787103028. |